Skip to main content

Posts

Showing posts with the label methali

Usirighe mundu usimudawa

 Usirighe mundu usimudawa. Kutoka: Deposit photos Picha: mtu anapiga shujaa wa dodi Usitusi mtu ambaye hujapiga. Kuchochea kwako kutakuletea maafa. Huwezi kuwa imara kwa shindano lolote. Watu wale wanadhaniwa bora wameishia kushindwa na watu waliodharauliwa katika shindano. #MethaliZaKilahaja 

Mundu ena ngingo teesowa kiraro

 Mundu ena ngingo teesowa kiraro Picha: Mtu aliye na mkeka Kutoka: Pexels.com   Mtu aliye na mkeka hakosi mahali pa kulala. Mkeka mzuri unaonekana kama kitu cha thamani. Maisha ni rahisi iwapo una uwezo wa kuishi katika mazingira yoyote. #MethaliZaKilahaja 

Kisimefwa usitaghe

 Kisimefwa usitaghe Asili: Pexels.com  Picha: Mtu anayeonyesha imani Usiache kuamini iwapo u hai. Maisha yamejaa pandashuka na hadithi za ufanisi baada ya uvumilivu. Kama kuna maisha na afya bora, basi kuna imani. Utaweza kubadilisha jambo iwapo utazidi kujaribu kila mara. #MethaliZaKilahaja 

Idio la mwana mkiwa lijimisha moto

 Idio la mwana mkiwa lijimisha moto Picha: Pexels  Methali hii ya Kitaveta inamaanisha hivi, kwa lugha ya kawaida, ndizi ya mtoto maskini italaumiwa kwa kuzima moto. Katika tukio ambalo linahusisha yatima aliyerithiwa na mtu wa karibu kama mjomba au shangazi. Moto unapozimika kijana anapochoma ndizi, basi ndizi ya ziada na uwepo wa kijana ndio utalaumiwa kwa kuharibu moto huo. Hutumika kama ukumbusho katika jamii ambapo aliye juu humwona aliye chini kama mtu anayekosea. #MethaliZaKilahaja 

Esikie mbeho niye esongeria moto

 Esikie mbeho niye esongeria moto.  Picha: Mtu anayehisi baridi Kutoka: Pexels.com  Mtu anayehisi baridi ndiye hufuata moto. Methali hii ya Kitaveta inadhihirisha kwamba: kabla hujahukumu mwanaume, tembea maili ndani ya viatu vyake. Huwezi kuelewa kabisa kile mtu anachopitia au sababu anavyoonyesha tabia ya kushangaza mpaka wewe uwekwe katika kama hali hio ndipo utaelewa.  #MethaliZaKilahaja 

Ng’ombe siru ina mkamiwe

 Ng’ombe siru ina mkamiwe Picha: Ng'ombe akikamuliwa.  Kutoka: Pexels.com   Ng'ombe aliyekasirika ana mtu wa kipekee wa kumkama. Hata watu walio na papara nyingi huwa na watu wanaoweza kuwatuliza. Methali hii inaweza kutumika kuwashauri wale wanatafuta wachumba. Wanashauriwa kutafuta wale wanapenda amani au wale wanagundua mazuri kutoka kwao. #MethaliZaKibantu