Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Kiswahili

Mofimu

     Mofimu Mofimu ni sehemu ndogo sana ya neno inayowasilisha maana. Kw mfano: katika neno 'Mgonjwa' 'm' ni mofimu ya kudhidhirisha umoja katika ngeli ya A - WA; 'Wa' katika "wagonjwa" ni mofimu ya wingi. - Mofimu aidha inaweza kuwa neno zima. Kwa mfano: Gari, Mama, Kisumu na Penseli. Mofimu huru Mifano ya mofimu huru - Mofimu huru ni ile inajisimamia bila usaidizi wowote. 1. Nomino. K.m Kuku, kiti, Uzi 2. Viwakilishi. K.m Mimi, sisi, wewe, nyinyi, yeye, wao 3. Vivumishi. K.m karimu, bora, nadhifu, humusi. 4. Viunganishi. K.m Mradi, sembuse Mofimu tegemezi /mofimu funge - Hizi hazina uwezo wa kujisimamia hadi ziongezewe viambishi awali.  K.m Kulima + m = mkulima          Ganga + m = mganga          Wete + ki = kiwete - Kuna mofimu funge ambazo zimepewa muundo wa majina mawili. K.m Mwana + mwali = mwanamwali          Mwana + nchi = mwananchi          Mwana + mkiwa = ...

Usirighe mundu usimudawa

 Usirighe mundu usimudawa. Kutoka: Deposit photos Picha: mtu anapiga shujaa wa dodi Usitusi mtu ambaye hujapiga. Kuchochea kwako kutakuletea maafa. Huwezi kuwa imara kwa shindano lolote. Watu wale wanadhaniwa bora wameishia kushindwa na watu waliodharauliwa katika shindano. #MethaliZaKilahaja 

Mundu ena ngingo teesowa kiraro

 Mundu ena ngingo teesowa kiraro Picha: Mtu aliye na mkeka Kutoka: Pexels.com   Mtu aliye na mkeka hakosi mahali pa kulala. Mkeka mzuri unaonekana kama kitu cha thamani. Maisha ni rahisi iwapo una uwezo wa kuishi katika mazingira yoyote. #MethaliZaKilahaja 

Kisimefwa usitaghe

 Kisimefwa usitaghe Asili: Pexels.com  Picha: Mtu anayeonyesha imani Usiache kuamini iwapo u hai. Maisha yamejaa pandashuka na hadithi za ufanisi baada ya uvumilivu. Kama kuna maisha na afya bora, basi kuna imani. Utaweza kubadilisha jambo iwapo utazidi kujaribu kila mara. #MethaliZaKilahaja 

Idio la mwana mkiwa lijimisha moto

 Idio la mwana mkiwa lijimisha moto Picha: Pexels  Methali hii ya Kitaveta inamaanisha hivi, kwa lugha ya kawaida, ndizi ya mtoto maskini italaumiwa kwa kuzima moto. Katika tukio ambalo linahusisha yatima aliyerithiwa na mtu wa karibu kama mjomba au shangazi. Moto unapozimika kijana anapochoma ndizi, basi ndizi ya ziada na uwepo wa kijana ndio utalaumiwa kwa kuharibu moto huo. Hutumika kama ukumbusho katika jamii ambapo aliye juu humwona aliye chini kama mtu anayekosea. #MethaliZaKilahaja 

Esikie mbeho niye esongeria moto

 Esikie mbeho niye esongeria moto.  Picha: Mtu anayehisi baridi Kutoka: Pexels.com  Mtu anayehisi baridi ndiye hufuata moto. Methali hii ya Kitaveta inadhihirisha kwamba: kabla hujahukumu mwanaume, tembea maili ndani ya viatu vyake. Huwezi kuelewa kabisa kile mtu anachopitia au sababu anavyoonyesha tabia ya kushangaza mpaka wewe uwekwe katika kama hali hio ndipo utaelewa.  #MethaliZaKilahaja 

Ng’ombe siru ina mkamiwe

 Ng’ombe siru ina mkamiwe Picha: Ng'ombe akikamuliwa.  Kutoka: Pexels.com   Ng'ombe aliyekasirika ana mtu wa kipekee wa kumkama. Hata watu walio na papara nyingi huwa na watu wanaoweza kuwatuliza. Methali hii inaweza kutumika kuwashauri wale wanatafuta wachumba. Wanashauriwa kutafuta wale wanapenda amani au wale wanagundua mazuri kutoka kwao. #MethaliZaKibantu

Sauti ghuna na sighuna

      Konsonanti ghuna ni sauti ambazo zinapotamkwa huwa kuna mtetemeko wa nyuzi sauti. Mifano  ya sauti ghuna ni : /z/, /b/, /g/, /d/, /gh/, /ny/, /ng/, /j/, /v/, /w/, /dh/, /y/, /n/, /m/. Konsonanti sighuna ni sauti ambazo zinapotamkwa huwa hakuna mtetemeko au mtikisiko wa nyuzi sauti.   Mifano  ya sauti sighuna ni: /s/, /k/, /t/, /p/, /ch/, /f/,  /h/, /th/.

Vinyume vya vielezi na vivumishi

 Japo vinyume katika sarufi ya Kiswahili hupatikana sana katika vitenzi, dhana hii hujitokeza katika vielezi na vivumishi pia. Vinyume vya vielezi 1. Mbali - karibu 2. Ndani - nje 3. Juu - chini 4. Haraka - polepole  Vinyume vya vivumishi 1. Mrefu - mfupi  2. Mnene - mwembamba 3. Safi - chafu 4. Mkubwa - mdogo 

Mifano ya viunganishi

  Mifano ya viunganishi 1. Ilhali. 2. Laiti 3. Minghairi ya 4. Maadamu 5. Aidha 6. Kwa niaba ya 7. Seuze  8. Sembuse 9. Hata 10. Kwa ajili ya 11. Kwa hivyo 12. Lau 13. Kwa mintarafu ya 14. Aghalabu 15. Mradi 16. Licha ya

Amba- na 'O' rejeshi

  Amba - na 'O' rejeshi Amba- na 'o' rejeshi havifuatani katika sentensi moja hasa kurejelea nomino moja.  Kwa mfano ni kosa kusema:   Mtoto ambaye aliyecheka anasoma. Sentensi sahihi ni: Mtoto ambaye alicheka anasoma.               au Mtoto aliyecheka anasoma.

Mfano wa Barua rasmi

  Shule ya Upili ya Mawejo, S.L.P. 657, Mawindoni. 7 /3/2024. Meneja, Kampuni ya Jebo, S.L.P. 5499, Jefule. Kwa Meneja, KUH: KUOMBA KAZI YA UHANDISI Kwa taadhima mkuu, ninaomba nafasi ya kazi ya Uhandisi katika kampuni yako. Nilipata habari hii kutoka kwa gazeti la Paruwaja iliyochapishwa tarehe 7/12/2023. Mimi ni mwanamke wa miaka ishirini na sita. Nimehitimu chuo kikuu cha Faragha katika taaluma hio. Aidha nimefanya kazi ya Uhandisi katika kampuni nyingi humu nchini. Katika kampuni hizo nimeonyesha utiifu, uwajibikaji na uwezo wa kubuni vitu vipya. Ukinipa nafasi hii, ninakuhakikisha mabadiliko katika sekta ya teknolojia. Nitakushukuru kwa kupata majibu yako baadaye.  Wako mwaminifu,  -^-^- Jerusha Tindo.

Barua rasmi

    Barua rasmi   Ni aina ya barua inayoandikwa kwa madhumuni ya shughuli za kiofisi au rasmi. Shughuli rasmi ni kama vile: kuomba nafasi ya ajira, kuomba radhi kwa kumkosea mtu, kuomba nafasi ya kutembea eneo fulani kama kituo cha redio au kuwataarifu wafanyikazi kuhusu mabadiliko katika kampuni. Vitu vya kuzingatia unapoandika barua rasmi. Hivi ndivyo vitu vinapaswa kuwa katika kila barua rasmi: 1. Anwani : barua rasmi huwa na anwani mbili; anwani ya mwandishi na anwani ya mwandikiwa. Anwani ya mwandishi hujumuisha makao ya mwandishi (shule, kijiji, ) , Sanduku la Posta (S.L.P.), Mji na tarehe ambayo barua inaandikwa. Anwani ya mwandikiwa inahusisha hivi: cheo au dhima ya mwandikiwa, sanduku la posta (S.L.P.) na Mji.  2. Anayeandikiwa barua rasmi . Katika sehemu hii, mtu anayeandikiwa hurejelewa kama: Kwa Bwana au Kwa Bibi . 3. Lengo Hii ndio sehemu ya tatu katika uandishi wa barua rasmi. Hapa ndipo madhumuni yanapoandikwa kwa ufupi. Kwa mfano: MINT: KUOMBA...

Aina za maghani simulizi

  Aina za maghani simulizi 1. Rara -> ni hadithi fupi na nyepesi aghalabu za kishairi zinazosimulia tukio la kuvutia na husimuliwa katika sherehe. 2. Ngano -> hii ni ngano ambayo inasimuliwa ikiandamana na ala za muziki badala ya kusimuliwa tu. 3. Sifo -> humsifu mhusika kwa kusimulia kwa kirefu matukio yanayoambatana na sifa zake. 4. Tendi -> ni masimulkzi marefu kuhusu mtu fulani mwenye sifa za ushujaa katika jamii au taifa nzima.

Lahaja

 Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainishwa na jamii au jiografia. Lahaja za lugha moja zinakaribiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati. Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi (upekee wa uzungumzaji), si lahaja. Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo: 1. vipengele vya sera (lahaja rasmi na lahaja sanifu) 2. vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika 3. vipengele vya kijamii (lahaja jamii na lahaja tabaka) 4. vipengele vya eneo

Hali na ukanusho

 Hali na ukanusho 1. Hali ya mazoea hu- Mifano: Wachache hupenda kusoma. -> Wachache hawapendi kusoma. Mkulima huhitaji maji mengi. -> Mkulima hahitaji maji mengi. Mvuvi huchelewa uvuvini. -> Mvuvi hachelewi uvuvuni. 2. Hali ya nge-, ngali- , ngeli-,  Mifano: Dereva angesoma vyema angepata maarifa. -> Dereva asingesoma vyema asingepata maarifa. Manamba angelichelewa kazini angelikosa unga. -> Manamba asingelichelewa kazini asingelikosa unga. Mjomba angalimtembelea mwanawe angalijua mengi. -> Mjomba asingalimtembelea mwanawe asingalijua mengi. 3. Hali ya -po- Mifano: Anapolima anapata uzoefu. -> Asipolima hapati uzoefu. Kilipojenga kilipendeza. -> kisipojengwa hakitapendeza. 4. Hali isiyodhihirika -a- Mifano: Acheza -> hachezi. Apigwa -> hapigwi. Ajenga -> hajengi. 5. Hali ya -ki- Mifano: Ukijitahidi utafanikiwa. -> usipojitahidi hutafanikiwa. Ukizembea utachelewa. -> usipozembea hutachelewa. ©️ Kelvin Munene  13/2/2024

Aina za viwakilishi

 Aina za Viwakilishi 1. Viwakilishi vya ngeli 2. Viwakilishi vya sifa 3. Viwakilishi vya idadi 4.Viwakilishi vimilikishi 5. Viwakilishi vya A- unganifu 6. Viwakilishi vya pekee 7. Viwakilishi vya 'O' rejeshi 8. Viwakilishi visisitizi

Vitenzi vya silabi moja

   Vitenzi vya silabi moja. Hivi humalizia na irabu 'a'. Zinapotumika katika sentensi kiambishi 'ku' huongezwa. Kwa mfano : fa --> kufa Kitenzi. Mzizi. Kauli ya kutendea La. L. Lia Pa. P. Pea Nywa. Nyw. Nywea Ja. J. Jia Fa. F. Fia Cha. Ch. Chia Pwa. Pw. Pwia Chwa. Chw. Chwea Wa. W. Wia Nya. Ny. Nyea.