Hali na ukanusho 1. Hali ya mazoea hu- Mifano: Wachache hupenda kusoma. -> Wachache hawapendi kusoma. Mkulima huhitaji maji mengi. -> Mkulima hahitaji maji mengi. Mvuvi huchelewa uvuvini. -> Mvuvi hachelewi uvuvuni. 2. Hali ya nge-, ngali- , ngeli-, Mifano: Dereva angesoma vyema angepata maarifa. -> Dereva asingesoma vyema asingepata maarifa. Manamba angelichelewa kazini angelikosa unga. -> Manamba asingelichelewa kazini asingelikosa unga. Mjomba angalimtembelea mwanawe angalijua mengi. -> Mjomba asingalimtembelea mwanawe asingalijua mengi. 3. Hali ya -po- Mifano: Anapolima anapata uzoefu. -> Asipolima hapati uzoefu. Kilipojenga kilipendeza. -> kisipojengwa hakitapendeza. 4. Hali isiyodhihirika -a- Mifano: Acheza -> hachezi. Apigwa -> hapigwi. Ajenga -> hajengi. 5. Hali ya -ki- Mifano: Ukijitahidi utafanikiwa. -> usipojitahidi hutafanikiwa. Ukizembea utachelewa. -> usipozembea hutachelewa. ©️ Kelvin Munene 13/2/2024