Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mofimu

Mofimu

     Mofimu Mofimu ni sehemu ndogo sana ya neno inayowasilisha maana. Kw mfano: katika neno 'Mgonjwa' 'm' ni mofimu ya kudhidhirisha umoja katika ngeli ya A - WA; 'Wa' katika "wagonjwa" ni mofimu ya wingi. - Mofimu aidha inaweza kuwa neno zima. Kwa mfano: Gari, Mama, Kisumu na Penseli. Mofimu huru Mifano ya mofimu huru - Mofimu huru ni ile inajisimamia bila usaidizi wowote. 1. Nomino. K.m Kuku, kiti, Uzi 2. Viwakilishi. K.m Mimi, sisi, wewe, nyinyi, yeye, wao 3. Vivumishi. K.m karimu, bora, nadhifu, humusi. 4. Viunganishi. K.m Mradi, sembuse Mofimu tegemezi /mofimu funge - Hizi hazina uwezo wa kujisimamia hadi ziongezewe viambishi awali.  K.m Kulima + m = mkulima          Ganga + m = mganga          Wete + ki = kiwete - Kuna mofimu funge ambazo zimepewa muundo wa majina mawili. K.m Mwana + mwali = mwanamwali          Mwana + nchi = mwananchi          Mwana + mkiwa = ...