Mofimu
Mofimu ni sehemu ndogo sana ya neno inayowasilisha maana.
Kw mfano: katika neno 'Mgonjwa' 'm' ni mofimu ya kudhidhirisha umoja katika ngeli ya A - WA; 'Wa' katika "wagonjwa" ni mofimu ya wingi.
- Mofimu aidha inaweza kuwa neno zima. Kwa mfano: Gari, Mama, Kisumu na Penseli.
Mofimu huru
Mifano ya mofimu huru
- Mofimu huru ni ile inajisimamia bila usaidizi wowote.
1. Nomino. K.m Kuku, kiti, Uzi
2. Viwakilishi. K.m Mimi, sisi, wewe, nyinyi, yeye, wao
3. Vivumishi. K.m karimu, bora, nadhifu, humusi.
4. Viunganishi. K.m Mradi, sembuse
Mofimu tegemezi /mofimu funge
- Hizi hazina uwezo wa kujisimamia hadi ziongezewe viambishi awali.
K.m Kulima + m = mkulima
Ganga + m = mganga
Wete + ki = kiwete
- Kuna mofimu funge ambazo zimepewa muundo wa majina mawili.
K.m Mwana + mwali = mwanamwali
Mwana + nchi = mwananchi
Mwana + mkiwa = mwanamkiwa
Comments
Post a Comment