Hali na ukanusho
1. Hali ya mazoea hu-
Mifano:
Wachache hupenda kusoma. -> Wachache hawapendi kusoma.
Mkulima huhitaji maji mengi. -> Mkulima hahitaji maji mengi.
Mvuvi huchelewa uvuvini. -> Mvuvi hachelewi uvuvuni.
2. Hali ya nge-, ngali- , ngeli-,
Mifano:
Dereva angesoma vyema angepata maarifa. -> Dereva asingesoma vyema asingepata maarifa.
Manamba angelichelewa kazini angelikosa unga. -> Manamba asingelichelewa kazini asingelikosa unga.
Mjomba angalimtembelea mwanawe angalijua mengi. -> Mjomba asingalimtembelea mwanawe asingalijua mengi.
3. Hali ya -po-
Mifano:
Anapolima anapata uzoefu. -> Asipolima hapati uzoefu.
Kilipojenga kilipendeza. -> kisipojengwa hakitapendeza.
4. Hali isiyodhihirika -a-
Mifano:
Acheza -> hachezi.
Apigwa -> hapigwi.
Ajenga -> hajengi.
5. Hali ya -ki-
Mifano:
Ukijitahidi utafanikiwa. -> usipojitahidi hutafanikiwa.
Ukizembea utachelewa. -> usipozembea hutachelewa.
©️ Kelvin Munene
13/2/2024
Comments
Post a Comment