Aina za Nomino
1. Nomino za jumla /kawaida - hizi ni zile ambazo hutaja kitu bila kukitambulisha kwa jina lake halisi.
K.m Kiatu, mti, gari
2. Nomino za pekee- ni maneno ambayo hutaja kitu kwa kukitambulisha waziwazi.
Kwa mfano: Bi. Onyancha, Mto Tana
3. Nomino dhahania
Ni majina ya vitu vya kufikirika tu wala haviwezi kugusika, kuonekana au kuonekana. Kwa mfano: uzembe, ulafi, uongo, wivu
4. Nomino za jamii
Ni majina ya vitu yanayotokea kwa makundi. Kila kundi hurejelewa kwa nomino maalum.
Kwa mfano:
Bunge litarejelea vikao mwezi ujao.
(Bunge; nomino ya jamii)
5. Nomino za wingi
Ni maneno ambayo hutokea katika hali ya wingi. Aidha, nomino hizo haziwezi kugawika ili ziwe kitu kimoja.
Kwa mfano: maji, unga
6. Nomino za kitenzi-jina
Ni vitenzi ambavyo vina kiambishi awali 'ku' na huwa vinatumika kama nomino.
Kwa mfano: Kutembea kwake kunafurahisha.
Facebook: https://www.facebook.com/KelvinMuneneOfficial
Email: kelvincreative3@gmail.com
WhatsApp: +254704406579
Comments
Post a Comment