Shamirisho ni sehemu fulani ya sentensi ambayo inayoonyesha kinachoathiriwa na nomino. Hutokea baada ya kitenzi kikuu.
Aina za Shamirisho
1. Shamirisho kipozi /Yambwa / Kitendwa /mtendwa
Hiki huonyesha kinachoathiriwa moja kwa moja.
K.m Paulo anacheza mpira.
(Mpira ---> shamirisho kipozi)
Hamisi ameshona kiatu.
(Kiatu ----> Shamirisho kipozi)
Wageni walituletea mahamri.
(Mahamri ----> shamirisho kipozi)
2. Shamirisho kitondo / Yambiwa / mtendewa /kitendewa
Huonyesha kinachoathiriwa kupitia kwa kitu kingine.
Kwa mfano:
Tunampikia mgeni mayai.
(Mgeni ----> shamirisho kitondo)
Amemchinjia Mwaliko kuku.
(Mwaliko ----> shamirisho kitondo)
Ninatayarishia Rashidi mkate.
(Rashidi ----> shamirisho kitondo)
3. Shamirisho Ala / kitumizi
Hiki huwa ni kifaa au kitu kinachowezesha kitenzi kufanyika.
Kwa mfano:
Anapika kwa mwiko.
(Kwa mwiko ---> shamirisho ala)
Nimechora ramani kwa penseli.
(Kwa penseli ----> shamirisho ala)
Wataletwa kwa basi.
(Kwa basi -----> shamirisho ala)
Chagizo: ni neno linatoa maelezo zaidi kuhusu kivumishi, kitenzi na kielezi kingine. Pia hueleza jambo litakavyofanyika, lilivyofanyika na linavyofanyika.
Kwa mfano:
Mamba atafika jioni.
(Jioni - chagizo)
Kingwena alikamatwa mwaka jana.
(Mwaka jana - chagizo)
Yohana anapika kwa kijiko.
(Kwa kijiko - chagizo)
Facebook: Kelvin Munene Official
Email: kelvincreative3@gmail.com
WhatsApp: +254704406579
Comments
Post a Comment