Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2023

Matumizi ya KI

    Matumizi ya Ki 'KI' ni kiambishi ambacho kinaweza kutumika katika mawanda tofauti ya sarufi ya Kiswahili. Mifano ya matumizi yake ni: 1. Katika udogo Kwa mfano : Kitoto, kijigombe, kidege. Mfano katika sentensi :  Kitoto kimechelewa kwenda shuleni. 2. Kuonyesha kiambishi ngeli ya Ki-Vi Kwa mfano : - Kiatu kimeraruka. - Chakula kimepikwa.  3. Katika ukanusho. Kwa mfano :  - Kasisi anacheka - Kasisi hacheki. 4. Katika nomino fulani za Kiswahili.   Kwa mfano : Kiswahili, kiraka, kinyume. 5. Kuonyesha lugha tofauti duniani.   Kwa mfano : Kiingereza, Kifaransa, Kilumi. 6. Kubainisha viashiria viradidi Kwa mfano : hiki hiki 7. Kuonyesha viashiria visisitizi. Kwa mfano : Kiki hiki 8. Kudhihirisha idadi. Kwa mfano : Mzigo huo ni kilo sita. (Neno 'kilo' limetumika kubainisha idadi.) 9. Kuonyesha nyakati.  Kwa mfano : Mkutano wa jumuia utaandaliwa kitondo. 10. Kuonyesha kielezi   Kwa mfano: -Mwangemi alichora kistadi. 11 . Kubanisha kitenzi kishiri...