Matumizi ya Ki
'KI' ni kiambishi ambacho kinaweza kutumika katika mawanda tofauti ya sarufi ya Kiswahili. Mifano ya matumizi yake ni:
1. Katika udogo
Kwa mfano: Kitoto, kijigombe, kidege.
Mfano katika sentensi:
Kitoto kimechelewa kwenda shuleni.
2. Kuonyesha kiambishi ngeli ya Ki-Vi
Kwa mfano:
- Kiatu kimeraruka.
- Chakula kimepikwa.
3. Katika ukanusho.
Kwa mfano:
- Kasisi anacheka - Kasisi hacheki.
4. Katika nomino fulani za Kiswahili.
Kwa mfano: Kiswahili, kiraka, kinyume.
5. Kuonyesha lugha tofauti duniani.
Kwa mfano: Kiingereza, Kifaransa, Kilumi.
6. Kubainisha viashiria viradidi
Kwa mfano: hiki hiki
7. Kuonyesha viashiria visisitizi.
Kwa mfano: Kiki hiki
8. Kudhihirisha idadi.
Kwa mfano:
Mzigo huo ni kilo sita.
(Neno 'kilo' limetumika kubainisha idadi.)
9. Kuonyesha nyakati.
Kwa mfano:
Mkutano wa jumuia utaandaliwa kitondo.
10. Kuonyesha kielezi
Kwa mfano:
-Mwangemi alichora kistadi.
11. Kubanisha kitenzi kishirikishi.
Kwa mfano:
- Kitabu ki mezani.
©️ Kelvin Munene 2023
Facebook: Kelvin Munene Official
WhatsApp: +254704406579
Comments
Post a Comment