Kirai ni fungu la maneno ambalo halina maana kamili. Huhitaji kuongezwa maneno mengine ili kuwasilisha maana.
Aina za virai
1. Kirai nomino - hutawaliwa na nomino. Nomino ndio hutangulia.
Aina za kirai nomino
(a). Nomino moja. Mfano: Mjomba amefika. ( Kirai nomino-> Mjomba.)
(b). Nomino mbili. Mfano: Ndovu na Simba wameuawa. (Kirai nomino-> Ndovu na Simba)
(c). Nomino na kivumishi. Mfano: Kiti kirefu kimenunuliwa. (Kirai nomino -> Kiti kirefu)
(d). Nomino na kundi-tenzi. Mfano: Upishi wa Zainabu ulioanza juzi umefutiliwa mbali. (Kundi nomino-> Upishi wa Zainabu ulioanza juzi)
2. Kirai Kitenzi
- Kitenzi ndicho kinachotangulia na kutawala.
Aina za kirai kitenzi
(a).Kitenzi pekee. Mfano: Waliochelewa wataadhibiwa. (Kirai kitenzi -> Waliochelewa)
(b). Kitenzi na nomino. Mfano: Aliyempa kalamu ametoroka. (Kirai kitenzi-> Aliyempa kalamu)
(c). Kitenzi na kitenzi. Mfano: Aliyemwakilisha amewasili ofisini. (Kirai kitenzi -> Aliyemwakilisha amewasili)
(d). Kitenzi-nomino na kitenzi. Mfano: Kupika kunapendeza wengi. (Kupika kunapendeza)
3. Kirai kivumishi
- Kivumishi ndicho hutangulia katika sentensi.
Aina za kirai kivumishi
(a). Kivumishi na kielezi chake. Mfano: Kitoto kijinga sana kitachapwa. (Kirai kivumishi-> kirai kivumishi)
(b). Kivumishi na nomino. Mfano: Shule yenye madarasa mengi imezinduliwa. (Kirai kivumishi -> Yenye madarasa)
(c). Kivumishi na kirai kitenzi. Mfano: Daktari mwenye hati mbaya ameajiriwa. (Kirai kivumishi-> Mwenye hati mbaya)
3. Kirai kielezi
- Kielezi ndicho hutangulia. Hueleza jinsi kitu kilivyofanyika mahali, wakati au mara ngapi.
Kwa mfano: Alfred alifika jana jioni.
Kirai kielezi -> jana jioni
4. Kirai kihusishi
- Kihusishi hutangulia kikifuatwa na nomino.
Kwa mfano: Lazima usimame mbele ya mgomba.
Kirai kihusishi -> mbele ya mgomba.
©️ Kelvin Munene 2023
Comments
Post a Comment