Kundi nomino ni sehemu ya sentensi iliyo na nomino pekee na maelezo ya nomino.
Aina za Kundi Nomino (KN)
1. Nomino pekee (KN -->N)
K.m Mwalimu anafunza.
KN --> N
N--> Mwalimu.
2. Nomino, kiunganishi na nomino (KN --> N + U + U)
K.m Nyanya na babu wanaimba.
KN -> N + U + U
N-> Nyanya
U -> na
N-> babu
3. Nomino na Kivumishi (KN -> N + V)
K.m Kijana mfupi ameenda nyumbani.
KN ->N + V
N-> Kijana
V -> mfupi
4. Nomino na vivumishi viwili (KN -> N + V+ V)
K.m Kiatu kipya cheupe kitanunuliwa.
KN-> N + V + V
N-> Kiatu
V -> kipya
V ->cheupe.
5. Nomino, kivumishi na kielezi (KN -> N+ V + E)
K.m Mtoto mrefu sana amekuja.
KN - N + V + E
N- Mtoto
V - mrefu
E - Sana.
6. Kiwakilishi pekee (KN ->W)
K.m Nyinyi mmenyamaza sana.
KN ->W
W - Nyinyi
7. Kiwakilishi, kiunganishi na kiwakilishi (KN -> W + U + W)
K.m Mimi na yeye ni maadui.
KN -> W + U + W
W -> Mimi
U -> na
W -> yeye.
8. Nomino na sentensi pungufu (KN -> N + ś )
K.m Pwagu aliyekamatwa juzi atachunguzwa.
KN -> N + ś)
N-> Pwagu
Ś-> aliyekamatwa juzi.
9. Kiwakilishi na sentensi pungufu (KN -> W + ś)
K.m Yule aliyetusalimia jana amepata jiko.
KN -> W + Ś
W -> Yule
Ś -> aliyetusalimia jana.
©️ Kelvin Munene 2023
Comments
Post a Comment