Matumizi ya "Ku"
1. Kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya mahali (KU - KU).
K.m Huku kunapendeza sana.
2. Kuanzisha vitenzi vya silabi moja au hali kamilifu ya kitendo.
K.m Anataka kuja.
3. Kuanzisha nomino za kitenzi jina.
K.m Kutembea kwake kutamchosha.
4. Kuanzisha vitenzi katika hali ya kawaida au kitenzi cha pili katika vitenzi sambamba.
K.m -Jembe hutumika kulima shamba.
- Tumezuru kwake kupiga gumzo.
5. Kiambishi cha kukanusha wakati uliopita.
K.m Chakula chako hakikupikika.
6. Kiambishi kiwakilishi cha mtendwa /mtendewa nafsi ya pili.
K.m Waganga watakutibu iwapo utafika mapema.
7. Kuonyesha mahali.
K.m Kuliko na zababu kunajengwa.
Comments
Post a Comment