Skip to main content

Matumizi ya "Kwa"

 Matumizi ya "kwa"


1.kuonyeshea kuwa chombo kinatumika kufanyia kazi.

Kwa mfano:

Mwalimu alipika chai kwa sufuria.



2. Kwa ya uhusiano wa mtu/watu na mahali .

Kwa mfano:

Hazina anazuru kwa Johana.


3. Kwa ya pamoja.

Kwa mfano:

Wazazi kwa watoto walilima shamba lao.


4. Kwa ya hali (kielezi).

Kwa mfano:

Jogoo alikimbia kwa upesi alipomwona mtetea.


-Aidha, Kwa inatumika huonyesha jinsi au namna jambo lilivyotendwa.

Kwa mfano:

Padri alihubiria kwa utaratibu.


5. Kwa ya kuonyeshea sehemu, kama vile katika aksami.

Kwa mfano:

Vijana watagawiwa tano kwa kumi.


6. Kwa ya unganifu - hutumika kwa vitenzi vilivyo na viambishi ku na nomino za mahali.

Kwa mfano:

Kusoma kwa Julia kunapendekezwa.


7. Kwa ya kiulizi na kwa ya kujibia. Mfano:

Digne: Kwa nini umenyamaza?


Maria: Kwa sababu ninahofia mwalimu mkuu.


8. Kwa ya nia/lengo au sababu .

Kwa mfano:

Nilitembea kwa arusi.


9. Kwa ya kimiliki cha nafsi ya kwanza (umoja) katika ngeli ya KU-KU.

Kwa mfano:

Nyumbani kwangu kunapendeza.




Comments