Muundo wa vitenzi
1. Vitenzi vya silabi moja
- Hivi huwa na silabi moja pekee. Hivi huongezewa kiungo KU katika kauli ya kutenda ili vilete maana.
Mifano ya vitenzi vya silabi moja.
1. - cha. Km. Kucha
2. - fa. Km. Kufa
3. - ja. Km. Kuja
4. - la. Km. Kula
5. - nya. Km. Kunya
6. - nywa. Km. Kunywa
7. - Pa. Km. Kupa
8. - Pwa. Km. Kupwa
9. - twa. Km. Kutwa
10. - Wa. Km. Kuwa
2. Vitenzi vya kigeni
- vina asili ya lugha nyingine badala ya kibantu. Baadhi ya lugha hizo ni: kireno, kihispania, kizungu, kiarabu.
- Havifuati muundo wa maneno mengi ya Kiswahili yanayoishia kwa sauti -a.
- Huishia na vokali hizi: - e, i, o, u.
Baadhi ya maneno ya kigeni ni: Samehe, baleghe, Shukuru, tubu, Keti.
3. Vitenzi vya kibantu
- Yana asili ya kibantu.
- Huishia na sauti ya vokali 'a'.
- Hujumuisha maneno mengi ya lugha ya Kiswahili.
K.m Kimbia, Ruka, Andika, Beba.
©️ Kelvin Munene 2023
Comments
Post a Comment