Skip to main content

Tanzu za Sarufi

  Tanzu za sarufi

1. Sarufi matamshi / fonolojia - hushughulikia matamshi ya vitamkwa kwa kuelekeza jinsi na mahali pa kutamkia katika kinywa cha msemaji.


2. Maumbo / mofolojia - herufi zinavyounganishwa kujenga maneno na kazi zake katika tungo.


3. Sarufi miundo / sintaksia - ni utanzu unaoshughulikia mpangilio au mfuatano wa maneno katika tungo ili yalete maana iliyokusudiwa.


4. Sarufi maana / semantiki - hujihusisha na maana mbalimbali za maneno na tungo za wazi. Aidha huelekeza namna ya kunguza tungo ili kupata maana, hasa iliyofichika.


5. Isimujamii - unajishughulisha na kaida na adabu ya matumizi ya lugha . Huelekeza aina ya lugha inayoruhusiwa kutumiwa na watu wa vyeo, umri, na hali mbalimbali katika muktadha na mazingira tofauti tofauti na kwa sababu maalumu.


©️ Kelvin Munene 2023

Comments