Ni kosa kutumia "kwa" kama kihusishi cha kitu au mahali; kwa + kitu au kwa + mahali.
K.m Enda kwa nyumba. --> (kwa + mahali)
Lala kwa kitanda. --> (kwa + kitu /mahali)
Tutaingia kwa lori. --> (kwa + mahali)
- Tunaposema 'enda kwa nyumba' , tunamaanisha kuwa nyumba ni mtu nawe unaambiwa uingie kwake.
Aidha, ni kosa kusema : Gari lilienda kwa kasi.
- Matumizi kama hayo yanafaa tu tunapomtaja mtu au watu.
K.m Utaishi kwa kaka.
- Kumbuka unapotaja mahali au kitu kuonyesha uhusiano au kihusishi, usitumie "kwa" tumia : 'kwenye' , "katika', 'ndani ya' au unatumia kiambishi tamati -ni.
©️ Kelvin Munene 2023
Comments
Post a Comment