Viambishi tamati
- Hutokea baada ya mzizi wa neno (shina la kitenzi)
- Hutekeleza majukumu yafuatayo ya kisarufi:
1. Mnyambuliko wa vitenzi
Kwa mfano: Pigika, Somesha. ( Mizizi = Pig-, Som-)
2. Viishio yakinifu vya vitenzi
Mfano: Walicheza. ('a' - kiishio)
3. Hali tofauti za kukanusha
Mfano: Siji (ji), Sili (Li)
4. "O" rejeahi tamati (mazoea)
Mfano: Kikulacho (cho), Alimaye (ye)
5. Viambishi vya mahali
Mfano: Kanisani (ni), Ajengapo (po)
6. Kuonyesha wingi, kuamuru au kuhimiza katika vitenzi
Mfano: Limeni! (ni), Njooni (ni)
7. Hali ya kuamrisha katika wingi
Mfano: Simameni (ni), Ketini
8. Amrisho katika hali ya ukanusho
Mfano: Usije, Usile.
Copyright. Kelvin Munene 2023
Comments
Post a Comment