Vivumishi vya pekee
1. - enye
Matumizi
(a) Kinaonyesha umilikaji
K.m - Mwenye gari lile hujishaua.
- Kiatu chenye tundu kitashonwa.
(b) Kuonyesha majina yanayotajwa yako katika hali fulani.
K.m Dawati lenye vitabu litauzwa.
2. - enyewe
Matumizi
(a) Kutilia mkazo hali fulani.
K.m Mkoba wenyewe ni mpya.
(b) Kuleta maana ya peke yake.
K.m Mwalimu mwenyewe aliwasili darasani.
3. - Ote
Kinaonyesha ujumla wa vitu.
K.m Wali wote umeliwa.
4. -O-O- te
Matumizi
(a) Kuonyesha hali ya kutofautisha vitu.
K.m Kazungu hapendi papai hili, ila atapenda lingine.
(b) Kuonyesha nyongeza ya vitu.
K.m Abdalla alioa bibi mwingine.
5. -ingineo
Huonyesha dhana ya 'zaidi ya'.
K.m Abdi alimnunulia mwanawe kanzu nyingineo.
©️ Kelvin Munene 2023
Comments
Post a Comment