Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2023

Aina za Nomino

  Aina za Nomino 1. Nomino za jumla /kawaida - hizi ni zile ambazo hutaja kitu bila kukitambulisha kwa jina lake halisi. K.m Kiatu, mti, gari 2. Nomino za pekee - ni maneno ambayo hutaja kitu kwa kukitambulisha waziwazi. Kwa mfano : Bi. Onyancha, Mto Tana 3. Nomino dhahania Ni majina ya vitu vya kufikirika tu wala haviwezi kugusika, kuonekana au kuonekana. Kwa mfano : uzembe, ulafi, uongo, wivu 4. Nomino za jamii Ni majina ya vitu yanayotokea kwa makundi. Kila kundi hurejelewa kwa nomino maalum.  Kwa mfano: Bunge litarejelea vikao mwezi ujao. (Bunge; nomino ya jamii) 5. Nomino za wingi Ni maneno ambayo hutokea katika hali ya wingi. Aidha, nomino hizo haziwezi kugawika ili ziwe kitu kimoja. Kwa mfano : maji, unga 6. Nomino za kitenzi-jina Ni vitenzi ambavyo vina kiambishi awali 'ku' na huwa vinatumika kama nomino. Kwa mfano: Kutembea kwake kunafurahisha. Facebook: https://www.facebook.com/KelvinMuneneOfficial Email : kelvincreative3@gmail.com  WhatsApp : +254704406579

Shamirisho na Chagizo

  Shamirisho ni sehemu fulani ya sentensi ambayo inayoonyesha kinachoathiriwa na nomino. Hutokea baada ya kitenzi kikuu. Aina za Shamirisho 1. Shamirisho kipozi /Yambwa / Kitendwa /mtendwa Hiki huonyesha kinachoathiriwa moja kwa moja. K.m Paulo anacheza mpira. (Mpira ---> shamirisho kipozi) Hamisi ameshona kiatu.  (Kiatu ----> Shamirisho kipozi) Wageni walituletea mahamri. (Mahamri ----> shamirisho kipozi) 2. Shamirisho kitondo / Yambiwa / mtendewa /kitendewa Huonyesha kinachoathiriwa kupitia kwa kitu kingine. Kwa mfano: Tunampikia mgeni mayai. (Mgeni ----> shamirisho kitondo) Amemchinjia Mwaliko kuku. (Mwaliko ----> shamirisho kitondo) Ninatayarishia Rashidi mkate. (Rashidi ----> shamirisho kitondo) 3. Shamirisho Ala / kitumizi Hiki huwa ni kifaa au kitu kinachowezesha kitenzi kufanyika. Kwa mfano: Anapika kwa mwiko. (Kwa mwiko ---> shamirisho ala) Nimechora ramani kwa penseli. (Kwa penseli ----> shamirisho ala) Wataletwa kwa basi. (Kwa basi -----> shamiris