Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2024

Vinyume vya vielezi na vivumishi

 Japo vinyume katika sarufi ya Kiswahili hupatikana sana katika vitenzi, dhana hii hujitokeza katika vielezi na vivumishi pia. Vinyume vya vielezi 1. Mbali - karibu 2. Ndani - nje 3. Juu - chini 4. Haraka - polepole  Vinyume vya vivumishi 1. Mrefu - mfupi  2. Mnene - mwembamba 3. Safi - chafu 4. Mkubwa - mdogo 

Mifano ya viunganishi

  Mifano ya viunganishi 1. Ilhali. 2. Laiti 3. Minghairi ya 4. Maadamu 5. Aidha 6. Kwa niaba ya 7. Seuze  8. Sembuse 9. Hata 10. Kwa ajili ya 11. Kwa hivyo 12. Lau 13. Kwa mintarafu ya 14. Aghalabu 15. Mradi 16. Licha ya

Amba- na 'O' rejeshi

  Amba - na 'O' rejeshi Amba- na 'o' rejeshi havifuatani katika sentensi moja hasa kurejelea nomino moja.  Kwa mfano ni kosa kusema:   Mtoto ambaye aliyecheka anasoma. Sentensi sahihi ni: Mtoto ambaye alicheka anasoma.               au Mtoto aliyecheka anasoma.

Mfano wa Barua rasmi

  Shule ya Upili ya Mawejo, S.L.P. 657, Mawindoni. 7 /3/2024. Meneja, Kampuni ya Jebo, S.L.P. 5499, Jefule. Kwa Meneja, KUH: KUOMBA KAZI YA UHANDISI Kwa taadhima mkuu, ninaomba nafasi ya kazi ya Uhandisi katika kampuni yako. Nilipata habari hii kutoka kwa gazeti la Paruwaja iliyochapishwa tarehe 7/12/2023. Mimi ni mwanamke wa miaka ishirini na sita. Nimehitimu chuo kikuu cha Faragha katika taaluma hio. Aidha nimefanya kazi ya Uhandisi katika kampuni nyingi humu nchini. Katika kampuni hizo nimeonyesha utiifu, uwajibikaji na uwezo wa kubuni vitu vipya. Ukinipa nafasi hii, ninakuhakikisha mabadiliko katika sekta ya teknolojia. Nitakushukuru kwa kupata majibu yako baadaye.  Wako mwaminifu,  -^-^- Jerusha Tindo.

Barua rasmi

    Barua rasmi   Ni aina ya barua inayoandikwa kwa madhumuni ya shughuli za kiofisi au rasmi. Shughuli rasmi ni kama vile: kuomba nafasi ya ajira, kuomba radhi kwa kumkosea mtu, kuomba nafasi ya kutembea eneo fulani kama kituo cha redio au kuwataarifu wafanyikazi kuhusu mabadiliko katika kampuni. Vitu vya kuzingatia unapoandika barua rasmi. Hivi ndivyo vitu vinapaswa kuwa katika kila barua rasmi: 1. Anwani : barua rasmi huwa na anwani mbili; anwani ya mwandishi na anwani ya mwandikiwa. Anwani ya mwandishi hujumuisha makao ya mwandishi (shule, kijiji, ) , Sanduku la Posta (S.L.P.), Mji na tarehe ambayo barua inaandikwa. Anwani ya mwandikiwa inahusisha hivi: cheo au dhima ya mwandikiwa, sanduku la posta (S.L.P.) na Mji.  2. Anayeandikiwa barua rasmi . Katika sehemu hii, mtu anayeandikiwa hurejelewa kama: Kwa Bwana au Kwa Bibi . 3. Lengo Hii ndio sehemu ya tatu katika uandishi wa barua rasmi. Hapa ndipo madhumuni yanapoandikwa kwa ufupi. Kwa mfano: MINT: KUOMBA...

Aina za maghani simulizi

  Aina za maghani simulizi 1. Rara -> ni hadithi fupi na nyepesi aghalabu za kishairi zinazosimulia tukio la kuvutia na husimuliwa katika sherehe. 2. Ngano -> hii ni ngano ambayo inasimuliwa ikiandamana na ala za muziki badala ya kusimuliwa tu. 3. Sifo -> humsifu mhusika kwa kusimulia kwa kirefu matukio yanayoambatana na sifa zake. 4. Tendi -> ni masimulkzi marefu kuhusu mtu fulani mwenye sifa za ushujaa katika jamii au taifa nzima.

Lahaja

 Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainishwa na jamii au jiografia. Lahaja za lugha moja zinakaribiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati. Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi (upekee wa uzungumzaji), si lahaja. Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo: 1. vipengele vya sera (lahaja rasmi na lahaja sanifu) 2. vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika 3. vipengele vya kijamii (lahaja jamii na lahaja tabaka) 4. vipengele vya eneo

Hali na ukanusho

 Hali na ukanusho 1. Hali ya mazoea hu- Mifano: Wachache hupenda kusoma. -> Wachache hawapendi kusoma. Mkulima huhitaji maji mengi. -> Mkulima hahitaji maji mengi. Mvuvi huchelewa uvuvini. -> Mvuvi hachelewi uvuvuni. 2. Hali ya nge-, ngali- , ngeli-,  Mifano: Dereva angesoma vyema angepata maarifa. -> Dereva asingesoma vyema asingepata maarifa. Manamba angelichelewa kazini angelikosa unga. -> Manamba asingelichelewa kazini asingelikosa unga. Mjomba angalimtembelea mwanawe angalijua mengi. -> Mjomba asingalimtembelea mwanawe asingalijua mengi. 3. Hali ya -po- Mifano: Anapolima anapata uzoefu. -> Asipolima hapati uzoefu. Kilipojenga kilipendeza. -> kisipojengwa hakitapendeza. 4. Hali isiyodhihirika -a- Mifano: Acheza -> hachezi. Apigwa -> hapigwi. Ajenga -> hajengi. 5. Hali ya -ki- Mifano: Ukijitahidi utafanikiwa. -> usipojitahidi hutafanikiwa. Ukizembea utachelewa. -> usipozembea hutachelewa. ©️ Kelvin Munene  13/2/2024