Skip to main content

Posts

Aina za maghani simulizi

  Aina za maghani simulizi 1. Rara -> ni hadithi fupi na nyepesi aghalabu za kishairi zinazosimulia tukio la kuvutia na husimuliwa katika sherehe. 2. Ngano -> hii ni ngano ambayo inasimuliwa ikiandamana na ala za muziki badala ya kusimuliwa tu. 3. Sifo -> humsifu mhusika kwa kusimulia kwa kirefu matukio yanayoambatana na sifa zake. 4. Tendi -> ni masimulkzi marefu kuhusu mtu fulani mwenye sifa za ushujaa katika jamii au taifa nzima.

Lahaja

 Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainishwa na jamii au jiografia. Lahaja za lugha moja zinakaribiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati. Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi (upekee wa uzungumzaji), si lahaja. Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo: 1. vipengele vya sera (lahaja rasmi na lahaja sanifu) 2. vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika 3. vipengele vya kijamii (lahaja jamii na lahaja tabaka) 4. vipengele vya eneo

Hali na ukanusho

 Hali na ukanusho 1. Hali ya mazoea hu- Mifano: Wachache hupenda kusoma. -> Wachache hawapendi kusoma. Mkulima huhitaji maji mengi. -> Mkulima hahitaji maji mengi. Mvuvi huchelewa uvuvini. -> Mvuvi hachelewi uvuvuni. 2. Hali ya nge-, ngali- , ngeli-,  Mifano: Dereva angesoma vyema angepata maarifa. -> Dereva asingesoma vyema asingepata maarifa. Manamba angelichelewa kazini angelikosa unga. -> Manamba asingelichelewa kazini asingelikosa unga. Mjomba angalimtembelea mwanawe angalijua mengi. -> Mjomba asingalimtembelea mwanawe asingalijua mengi. 3. Hali ya -po- Mifano: Anapolima anapata uzoefu. -> Asipolima hapati uzoefu. Kilipojenga kilipendeza. -> kisipojengwa hakitapendeza. 4. Hali isiyodhihirika -a- Mifano: Acheza -> hachezi. Apigwa -> hapigwi. Ajenga -> hajengi. 5. Hali ya -ki- Mifano: Ukijitahidi utafanikiwa. -> usipojitahidi hutafanikiwa. Ukizembea utachelewa. -> usipozembea hutachelewa. ©️ Kelvin Munene  13/2/2024

Aina za viwakilishi

 Aina za Viwakilishi 1. Viwakilishi vya ngeli 2. Viwakilishi vya sifa 3. Viwakilishi vya idadi 4.Viwakilishi vimilikishi 5. Viwakilishi vya A- unganifu 6. Viwakilishi vya pekee 7. Viwakilishi vya 'O' rejeshi 8. Viwakilishi visisitizi

Vitenzi vya silabi moja

   Vitenzi vya silabi moja. Hivi humalizia na irabu 'a'. Zinapotumika katika sentensi kiambishi 'ku' huongezwa. Kwa mfano : fa --> kufa Kitenzi. Mzizi. Kauli ya kutendea La. L. Lia Pa. P. Pea Nywa. Nyw. Nywea Ja. J. Jia Fa. F. Fia Cha. Ch. Chia Pwa. Pw. Pwia Chwa. Chw. Chwea Wa. W. Wia Nya. Ny. Nyea. 

Sifa za Tamthilia

 Tamthilia ni mchezo wa kuigiza uliondikwa. Ukweli ni kwamba, tamthilia zote zinasheheni elimu kwa wanajamii kwa kufichua uozo uliokithiri.  Sifa za tamthilia 1. Wahusika hujibizana. Tamthilia ni kama dayolojia iliyokomaa. 2. Kuna matumizi ya mabano. Kwa mfano: (akicheka). Maneno hayo yaliyofungiwa ndiyo muigizaji huzingatia anapoigiza jukwaani. 3. Huwa na maneno kama elfu 10,000 hadi 20,000 japo yanaweza kuwa mengi au machache. Jumla ya maneno huwa hivyo. ©️ Kelvin Munene Official 

Matumizi ya NA

   Matumizi ya 'Na' 1. Kuonyesha kiunganishi.  Kwa mfano: Joshua na Becky watachapwa. 2. Hutumika katika mnyambuliko wa vitenzi. Kwa mfano: Piga -->pigana , pigiana 3. Kuonyesha wakati uliopo. Kwa mfano: Juma anasoma. 4. Kuorodhesha Kwa mfano: Keziah amenunua mayai, mboga, baiskeli na mahindi.

Matumizi ya "ni"

    Matumizi ya 'ni' 1. Kubainisha mahali. Kwa mfano: nyumbani, darasani. 2. Kuonyesha kitenzi kishirikishi kipungufu. Kwa mfano: Yohana ni mkimbiaji. 3. Kubainisha nafsi ya kwanza. Kwa mfano: Nitamtembelea. 4. Ukanusho. Kwa mfano: Mathayo hapendani. 5. Baadhi ya nomino za Kiswahili.  Kwa mfano: Nikaha. 6. Kuonyesha kielezi. Kwa mfano: Yusufu alimtembelea shambani. 7. Kubainisha upande. Kwa mfano: Kaskazini, kusini.

Matumizi ya "Kwa"

 Matumizi ya "kwa" 1.kuonyeshea kuwa chombo kinatumika kufanyia kazi. Kwa mfano: Mwalimu alipika chai kwa sufuria. 2. Kwa ya uhusiano wa mtu/watu na mahali . Kwa mfano: Hazina anazuru kwa Johana. 3. Kwa ya pamoja. Kwa mfano: Wazazi kwa watoto walilima shamba lao. 4. Kwa ya hali (kielezi). Kwa mfano: Jogoo alikimbia kwa upesi alipomwona mtetea. -Aidha, Kwa inatumika huonyesha jinsi au namna jambo lilivyotendwa. Kwa mfano: Padri alihubiria kwa utaratibu. 5. Kwa ya kuonyeshea sehemu, kama vile katika aksami. Kwa mfano: Vijana watagawiwa tano kwa kumi. 6. Kwa ya unganifu - hutumika kwa vitenzi vilivyo na viambishi ku na nomino za mahali. Kwa mfano: Kusoma kwa Julia kunapendekezwa. 7. Kwa ya kiulizi na kwa ya kujibia. Mfano: Digne: Kwa nini umenyamaza? Maria: Kwa sababu ninahofia mwalimu mkuu. 8. Kwa ya nia/lengo au sababu . Kwa mfano: Nilitembea kwa arusi. 9. Kwa ya kimiliki cha nafsi ya kwanza (umoja) katika ngeli ya KU-KU. Kwa mfano: Nyumbani kwangu kunapendeza.

Tanzu za Sarufi

  Tanzu za sarufi 1. Sarufi matamshi / fonolojia - hushughulikia matamshi ya vitamkwa kwa kuelekeza jinsi na mahali pa kutamkia katika kinywa cha msemaji. 2. Maumbo / mofolojia - herufi zinavyounganishwa kujenga maneno na kazi zake katika tungo. 3. Sarufi miundo / sintaksia - ni utanzu unaoshughulikia mpangilio au mfuatano wa maneno katika tungo ili yalete maana iliyokusudiwa. 4. Sarufi maana / semantiki - hujihusisha na maana mbalimbali za maneno na tungo za wazi. Aidha huelekeza namna ya kunguza tungo ili kupata maana, hasa iliyofichika. 5. Isimujamii - unajishughulisha na kaida na adabu ya matumizi ya lugha . Huelekeza aina ya lugha inayoruhusiwa kutumiwa na watu wa vyeo, umri, na hali mbalimbali katika muktadha na mazingira tofauti tofauti na kwa sababu maalumu. ©️ Kelvin Munene 2023

Matumizi ya "Ku"

  Matumizi ya "Ku" 1. Kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya mahali (KU - KU). K.m Huku kunapendeza sana. 2. Kuanzisha vitenzi vya silabi moja au hali kamilifu ya kitendo. K.m Anataka kuja. 3. Kuanzisha nomino za kitenzi jina. K.m Kutembea kwake kutamchosha. 4. Kuanzisha vitenzi katika hali ya kawaida au kitenzi cha pili katika vitenzi sambamba. K.m -Jembe hutumika kulima shamba.         - Tumezuru kwake kupiga gumzo. 5. Kiambishi cha kukanusha wakati uliopita. K.m Chakula chako hakikupikika. 6. Kiambishi kiwakilishi cha mtendwa /mtendewa nafsi ya pili. K.m Waganga watakutibu iwapo utafika mapema. 7. Kuonyesha mahali. K.m Kuliko na zababu kunajengwa.

Matumizi ya "Ka"

   Matumizi ya "ka" 1. Kiambishi kiwakilishi cha wakati usiodhihirika. K.m Mjomba akamtuma mwanawe dukani anunue vibanzi. 2. Katika vitenzi sambaba. K.m Tulienda mtoni kisha tukabeba nyasi. 3. Kuagiza. K.m Kamwambie anahitajika nyumbani.  4. Kuamuru. K.m Kasome! Kijiji hakitupendi sana. 5. Kiishio cha kauli ya kutendeka. K.m Halima alijaribu kumtongoza Juma lakini hakupendeka.

Matumizi ya "Ji"

  Matumizi ya "Ji" 1. Kuonyesha hali ya ukubwa katika umoja. K.m Mtu - Jiti, Mti - Jiti. 2. Hutumika kama kiambishi kirejeshi kinachoonyesha kuw mtu amejitendea kitendo husika yeye mwenyewe. K.m Amejitega. 3. Hutumika mwishoni mwa nomino kuonyesha hali ya mazoea. K.m Msomaji, mchekeshaji. 4. Kudharau. K.m Jitoto hilo linacheka. 5. Hutumika kama kiambishi cha urejeshi wa nafsi. K.m Tulijipikia chakula chetu.

Matumizi ya "Katika"

  Matumizi ya 'katika' 1. Kuonyesha uhusiano  wa mahali. K.m Bosire atakuwa katika gari lake.  2. Kuonyesha undani wa mahali badala ya kiambishi 'ni'. K.m Dereva ameingia katika basi. 3. Kuonyesha hali fulani. K.m Wamekuwa katika hali tatanishi.

Matumizi ya Jinsi

  Matumizi ya "jinsi" 1. Kuaminisha aina au sampuli. K.m Mradi wa jinsi hii hautapendwa. 2. Hutumika kuleta maana ya namna au jinsi ya kutenda jambo. K.m Tunafahamu jinsi ya kulima maharagwe.  3. Hutumika kumaanisha vile kitendo kilifanywa. K.m Hakujua jinsi aliibiwa na bintiye.

Matumizi ya "namna "

  Matumizi ya "namna" 1. Kuonyesha njia ya kufanya jambo. K.m Nanjala anafahamu namna ya kupika ugali. 2. Kuleta maana ya 'vile'. K.m Namna alivyoning'ata ungedhani nilimkosea sana. 3. Kuonyesha aina au sampuli. K.m Chakula cha namna hii si kizuri.

Matumizi ya walakini

  Matumzi ya 'walakini' 1. Hutimika kuonyesha maana ya "hata hivyo" au "ila". K.m Selume alisoma kwa miaka mingi walakini alifanikiwa baadaye. 2. Hutumika kuonyesha maana ya 'kasoro' au 'dosari'. K.m Kitabu hiki kina walakini, kinafaa kubadilishwa.

Vivumishi vya pekee

  Vivumishi vya pekee 1. - enye     Matumizi (a) Kinaonyesha umilikaji K.m - Mwenye gari lile hujishaua.        - Kiatu chenye tundu kitashonwa. (b) Kuonyesha majina yanayotajwa yako katika hali fulani. K.m Dawati lenye vitabu litauzwa. 2. - enyewe   Matumizi (a) Kutilia mkazo hali fulani. K.m Mkoba wenyewe ni mpya. (b) Kuleta maana ya peke yake. K.m Mwalimu mwenyewe aliwasili darasani. 3. - Ote Kinaonyesha ujumla wa vitu. K.m Wali wote umeliwa. 4. -O-O- te Matumizi  (a) Kuonyesha hali ya kutofautisha vitu. K.m Kazungu hapendi papai hili, ila atapenda lingine. (b) Kuonyesha nyongeza ya vitu. K.m Abdalla alioa bibi mwingine.  5. -ingineo Huonyesha dhana ya 'zaidi ya'. K.m Abdi alimnunulia mwanawe kanzu nyingineo. ©️ Kelvin Munene 2023