Muundo wa vitenzi 1. Vitenzi vya silabi moja - Hivi huwa na silabi moja pekee. Hivi huongezewa kiungo KU katika kauli ya kutenda ili vilete maana. Mifano ya vitenzi vya silabi moja. 1. - cha. Km. Kucha 2. - fa. Km. Kufa 3. - ja. Km. Kuja 4. - la. Km. Kula 5. - nya. Km. Kunya 6. - nywa. Km. Kunywa 7. - Pa. Km. Kupa 8. - Pwa. Km. Kupwa 9. - twa. Km. Kutwa 10. - Wa. Km. Kuwa 2. Vitenzi vya kigeni - vina asili ya lugha nyingine badala ya kibantu. Baadhi ya lugha hizo ni: kireno, kihispania, kizungu, kiarabu. - Havifuati muundo wa maneno mengi ya Kiswahili yanayoishia kwa sauti -a. - Huishia na vokali hizi: - e, i, o, u. Baadhi ya maneno ya kigeni ni: Samehe, baleghe, Shukuru, tubu, Keti. 3. Vitenzi vya kibantu - Yana asili ya kibantu. - Huishia na sauti ya vokali 'a'. - Hujumuisha maneno mengi ya lugha ya Kiswahili. K.m Kimbia, Ruka, Andika, Beba. ©️ Kelvin Munene 2023